• Huduma kwa wateja: +255 657 907 091
 • KARIBU CHOLEMU INVESTMENT LTD
  Kwa
  Mahitaji ya
  Mashamba
  Viwanja
  Upimaji
 • TupoTayari
  Kukuhudumia
  Tupigie sasa
  +255 657 907 091
HISTORIA YA KAMPUNI

Cholemu Investment ltd.

Cholemu investment limited ni kampuni iliyoanzishwa mwaka 2017 jijini dar es salaam na kusajiliwa chini ya sheria ya makampuni ya mwaka 2002 nchini tanzania na baadae kupata kibali cha kufanya shughuli za upimaji na uuzaji wa ardhi kwa watu binafsi, vikundi na taasisi ndani ya eneo lote la nchi ya tanzania. Kampuni yetu inatoa huduma hizo tajwa kwa njia ya mikopo nafuu isiyokuwa na riba wala dhamana.

Mwalimu Julius K. Nyerere aliwahi kunukuliwa akisema kwamba, “Ili tuendelee tunahitaji vitu vinne katika kuchangia maendeleo, vitu hivyo ni ardhi, siasa safi,uongozi bora na watu”. Kwa msingi huu mwalimu aliweka wazi juu ya umuhimu wa kumiliki ardhi. Moja ya misingi mikuu ya ardhi ni raia wote wanawake na wanaume kuwa na haki sawa ya kupata, kumiliki, kutumia na kugawa ardhi. Hivyo kampuni ya Cholemu Investment Limited imejikita zaidi katika kuhakikisha kila mtanzania anamiliki ardhi iliyopimwa.

Huduma zetu

Cholemu investment limited imejikita katika utoaji wa huduma mbali mbali zinazohusiana na masuala mazima ya ardhi
bg-image

Ufafanuzi Kuhusiana Na Ardhi

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Aliwahi Kunukuliwa Akisema Kwamba, Ili Tuendelee Tunahitaji Vitu Vinne Katika Kuchangia Maendeleo. Vitu Hivyo Ni Ardhi, Siasa Safi, Uongozi Bora Na Watu. Kwa Msingi Huu Mwalimu Alimaanisha Kwamba, Ardhi Ni Miongoni Mwa Misingi Madhubuti Ya Maendeleo. Hivyo Basi, Kama Wananchi Watapatiwa Ardhi Kwa Kadiri Inavyotakikana Na Kuitumia Kwa Ufanisi Basi Ardhi Itawakwamua Kiurahisi Katika Wimbi La Umasikini Na Kuwasaidi Kuwa Na Rasilimali Ya Kutosha Kwa Ajili Yao Na Vizazi Vijavyo. Kwa Mujibu Wa Sheria Ya Ardhi Ya Mwaka 2002; Ardhi Inajumuisha Nafasi Ya Juu Ya Ardhi Pamoja Na Ile Iliyopo Chini Yake Na Vitu Vyote Vilivyomo Ndani Yake Isipokuwa Madini Au Mafuta Yaliyopo Katika Ardhi Hiyo. Hii Inajumuisha Pia Vitu Vya Asili Vinavyoota Au Kuoteshwa Katika Ardhi Hiyo, Majengo Pamoja Na Ardhi Iliyofunikwa Na Maji. Sheria Hii Paoja Na Sera Na Kanuni Zake Zinaeleza Kwamba Ardhi Yote Ya Tanzania Ni Mali Ya Umma Ikiwa Chini Ya Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Kama Mdhamini Kwa Niaba Ya Wananchi Na Kuhakikisha Kuwa Haki Zilizopo Au Umiliki Ambao Umekuwepo Tangu Awali Unatambuliwa Na Kulindwa.

Umiliki Wa Ardhi Kwa Mujibu Wa Sheria

Kwa Mujibu Wa Sheria Za Ardhi, Kila Raia Wa Tanzania Ana Haki Ya Kumiliki Ardhi. Kumilikishwa Ardhi Si Hisani Bali Ni Haki Ya Kila Raia Ya Kisheria Na Kikatiba. Hivyo Kila Mwananchi Anapaswa Kuonyeshwa Na Kuwezeshwa Ni Kwa Jinsi Gani Ataweza Kumiliki Ardhi.

Tanzania Ni Nchi Iliyobahatika Sana Miongoni Mwa Nchi Zilizo Katika Eneo La Afrika Mashariki Kwa Kuwa Na Ardhi Tele Ambayo Kila Raia Wa Kizazi Cha Sasa Na Kijacho Anao Uwezo Wa Kumiliki Ardhi Pasipo Na Tatizo Lolote. Takwimu Za Kitafiti Zinaonyesha Kwamba Katika Nchi Tano Za Afrika Mashariki 51% Ya Eneo La Ardhi Linachangiwa Na Ardhi Kutoka Nchi Ya Tanzania, Hii Inatoa Picha Ni Kwa Namna Gani Kuna Utajiri Wa Ardhi Katika Nchi Hii Kwa Raia Wake.

bg-image

Wateja/Walengwa

Wateja ambao tumewalenga katika biashara hii ya uuzaji wa viwanja vilivyopimwa kwa njia ya mikopo ni watanzania wote wenye umri wa miaka 18 au zaidi. Pia tunauza maeneo kwa taasisi binafsi, mashirika ya kimataifa na NGOs
Switcher Colors